Mfuko wa TASAF watoa jumla ya shillingi bilioni 20 mkoani Tabora.
![]() |
Tanzania Social Action Fund (TASAF) |
TABORA yanufaika na mfuko wa TASAF.
Jumla ya shilingi bilioni 20 zimetolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Halmashhauri zote za Tabora kwa ajili kunusuru kaya maskini katika eneo hilo.
Hayo yamesemwa mjini Tabora na Mratibu wa TASAF mkoa huo, Ngoko Buka wakati wa kikao cha kutathmini utekelezaji wa TASAF Awamu ya Tatu sehemu ya kwanza kilichowashirikisha Wafadhili ,viongozi kutoka makao Makuu TASAF na wale wa Mkoa na Wilaya ya Uyui.
Amesema kuwa fedha hizo zilitolewa katika kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Agosti mwaka huu ambapo jumla ya walengwa 45,928 waliwezwa kunufaika na fedha hizo na hatimaye kubadilisha maisha yao.
Aidha, ameongeza kuwa fedha zimesaidia baadhi ya walengwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ufugaji wa kuku,bata,mbuzi ,ng’ombe ,ujenzi wa nyumba bora, kusomesha watoto, kuwapa huduma ya kliniki na kuimarisha kilimo
Hata, kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa TASAF kutoka Makao Makuu Dkt. Jasson Bagonza alisema kuwa wako mkoani Tabora kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoratibiwa na Mfuko huo na kujadiliana na wadau mbalimbali ili kuona kama inakwenda malengo ya uanzishaji wake.
No comments:
Post a Comment