Mikopo awamu ya pili kutoka bodi ya mikopo (HESLB) soma kwa haraka zaidi hapa
MIKOPO YA WANAFUNZI WA VYUO AWAMU YA PILI 2017-2018
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya awamu ya pili ya wanafunzi 11,481 wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa kupata mikopo.
Orodha hiyo ya wanafunzi ya awamu ya pili inapatikana kwenye tovuti hii (www.heslb.go.tz) na itatumwa kwa vyuo husika.
Vilevile, tunawafahamisha wanafunzi wanaoendelea na masomo na umma kwa ujumla kuwa tunaendelea kutuma vyuoni majina na fedha za mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wamefaulu mitihani yao.
No comments:
Post a Comment