TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI BENJAMIN MKAPA HOSPITAL.
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na EA.7/96/01/J/68 17 Novemba, 2017
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Benjamin Mkapa Hospital anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 29-30 Novemba, 2017 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye Usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 29-30 Novemba, 2017 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, muda wa Usaili umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-Kitambulisho cha Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
v. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha IV na VI (Results Slips) HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA); na
ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya Tangazo husika.
x. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na Vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.>>Gusa hapa kusoma majina ya walioitwa kwenye usaili
No comments:
Post a Comment