Header Ads

JESHI LA ZIMBABWE LACHUKUA MADARAKA YA NCHI HIYO. MUGABE BADO HAJULIKANI ALIPO.


Jeshi la nchi ya Zimbabwe linaripotiwa kuchukua madaraka ya nchi hiyo huku Rais Robert Mugabe asijulikane alipo pamoja na mke wake. Awali mapema asubuhi hii, vifaru vya jeshi hilo vilionekana kuzunguka katika mji wa Harare nchini humo.

Pamoja na yote hayo, mkuu wa jeshi la nchi hiyo amekanusha kuwa kinachoendelea nchini humo sio MAPINDUZI YA KIJESHI ingawa wanasiasa wengi wanadiriki kuita hivyo. Jeshi hilo linadai kuwa limeingilia kati utawala wa Rais Mugabe ili kukabiliana na wapinzani wa Mugabe na kuhakikisha usalama wa Rais huyo.

Mnamo mapema wiki hii, mkuu wa jeshi hilo aligusia kwamba wataingilia kati migogoro ya kisiasa nchini humo ambayo inasababisha kuyumba kwa uchumi wa nchi hiyo. Migogoro hii mikubwa inaibuka hasa baada ya Rais Mugabe kumfukuza kazi msaidizi wake ambaye inaonekana anaungwa mkono na jeshi la nchi hiyo

Pamoja na hayo, hapo awali ilijulikana kuwa Rais Mugabe alitaka kumuachia mke wake madaraka ya nchi hiyo jambo ambalo lilistua mioyo ya wananchi wengi wa Zimbabwe na dunia nzima kwa ujumla. Pengine hiki ndio kinasadikiwa kuwa ndio chanzo cha jeshi kuingilia kati utawala huo.

Mpaka sasa haijulikani ni wapi Mugabe na mke wake wapo.

No comments: