Header Ads

KUITWA KAZINI WALIOSAILIWA OKTOBA NA KUPATA KAZI MNH, MOI, TFS, GCL, LGTI, KCMC & EASTC



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/J/64
08 Novemba, 2017


TANGAZO LA KUITWA KAZINI



Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),Taasisi ya Mifupa (MOI), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wakala wa
Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Chuo cha Serikali za Mitaa– Hombolo (LGTI), Hospitali ya Rufaa ya KCMC na Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC) waliofanya usaili kuanzia tarehe 17 – 27 Oktoba, 2017 kuwa matokeo ya usaili yamekwishaidhinishwa na waombaji kazi waliofaulu usaili huo na kupendekezwa kutumwa kwa Mwajiri ni kama yalivyoorodheshwa katika Tangazo hili.

2. Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo Barabara ya Bibi Titi Mohamed, Jengo la Maktaba Kuu ya Taifa,
ghorofa ya pili, Masjala ya wazi ndani ya siku 7 kutoka tarehe ya tangazo hili, baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.



3. Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) za
masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya
kupewa barua ya Ajira.


4. Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.


No comments: