Header Ads

MSIMAMO WA ACT WAZALENDO KUJIUNGA NA UKAWA

ACT WAZALENDO 


Chama cha ACT Wazalendo kimeweka wazi msimamo wake kuhusu suala la kujiunga na UKAWA ambapo kimesema suala hilo ni pana na lazima lizingatie maslahi ya chama. Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho Ado Shaibu, amesema suala la kujiunga au kutojiunga UKAWA litaamuliwa na wanachama na viongozi. “Ni kweli kila mtu anazungumza yake kuhusu msimamo wa chama chetu lakini ukweli ni kwamba kwa hali ya kisiasa ilivyo nchini kuna mambo yanalazimu vyama vya upinzani vishirikiane, lakini ikija suala la kujiunga UKAWA lazima ujue maslahi ya chama ndani ya umoja huo”, amesema Ado Shaibu.

Nini maoni yako? Tuandikie hapo chini kwenye kisanduku 

No comments: