Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akabidhi barua ya kujiuzulu nafasi ya Urais nchini Zimbabwe.
Harare, Zimbabwe
Rais wa Robert Mugabe wa Zimbabwe amekabidhi barua ya kujiuzulu wadhifa wake katika bunge la nchi hiyo.
Hatua hiyo imekuja muda mchache baada ya Bunge la Zimbabwe kukutana kwa lengo la kuanza taratibu za kupiga kura ya kumuondoa madarakani Rais huyo.
Mugabe amekua madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mwaka 1980. zimbabwe imejikuta katika mgogoro wa kisiasa baada ya Rais Robert Mugabe kumfukuza makamu wa Rais wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa wiki chache zilizopita.
Source: TBCHabari
No comments:
Post a Comment