Header Ads

WANAFUNZI WATANO WAHOFIWA KUFA NA WENGINE KUJERUHIWA SABABU YA MLIPUKO WA BOMU



Ngara, Kagera

Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni wa bomu umepelekea vifo vya wanafunzi watatu na kujeruhi wengine kadhaa katika Shule ya Msingi Kihinga wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Inasemekana kuwa kulikuwa na uuzaji wa vyuma chakavu, hivyo baada ya mapumziko ya vipindi (saa 4 asubuhi) vijana wakaenda kuuza kumbe ni bomu na baada ya muda katika kipindi cha uuzaji likalipuka, mpaka sasa inasadikiwa wanafunzi watano wamefariki na wengine 20 wamejeruhiwa na wamepumzishwa katika hospitali ya Rulenge.

Source: Swahili Times

No comments: