#ZIMBABWE: RAIS ROBERT MUGABE HAYUKO TAYARI KUACHIA MADARAKA.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amesema kuwa yeye bado ni kiongozi halali wa nchi hiyo na kukataa upatanishi unaofanywa na Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki ili kuwezesha mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani baada ya jeshi kuchukua udhibiti tangu siku ya Jumatano. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini humo, Kasisi Fidelis Mukonori, amejitolea kuwa mpatanishi kati ya Majenerali wa Jeshi na Rais Mugabe, ingawa hakuna taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo yenye lengo la kuepusha umwagaji damu baada ya Mugabe kuondoka madarakani.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amekataa wito unaomtaka ajiuzulu kwa hiari yake kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.Rais Mugabe ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 93 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani wakati jeshi lilipochukua madaraka siku ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment