MABASI YALIYOKUWA YANASAFIRISHA WAKIMBIZI KWENDA BURUNDI YAPATA AJARI MBAYA WILAYANI NGARA, WATU KADHAA WAHOFIWA KUFA NA WENGINE KUJERUHIWA. CLICK
![]() |
| Moja ya gari lililopata ajari. |
Kwenye ajali hiyo, watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha yao huku idadi ya majeruhi ikiwa kubwa mno. Majeruhi wamepelekwa Hospitali ya wilaya ya Ngara, NYAMIAGA na wengine wamepelekwa hospitali ya Murgwanza wilayani Ngara.
Aidha, idadi ya watoto kwenye ajali hiyo ndio imekuwa kubwa kuliko watu wazima, mwandishi wa Blog hii WWW.KALUNDE.CO ameshuhudia majeruhi katika hospitali ya Murgwanza na kwamba wengine hali zao zilikuwa mbaya sana.
KALUNDE BLOG iliongea na madereva wawili walionusurika kwenye ajali hiyo wakiwa hospitali ya Murugwanza na walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ilikuwa basi moja kujaribu kulipita basi lingine na kisha kuparamia gari lingine, idadi ya mabasi yote kwa ujumla kwa taarifa za majeruhi mmoja yalikuwa nane.
![]() |
| Miongoni mwa magari yaliyokuwa yanasafirisha wakimbizi hao. |
...INAENDELEA
Kwenye ajali hiyo watu watano wamefariki na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amethibitisha. Kati yao, watatu ni wanawake na miongoni mwao wanaume mmoja alikuwa anaendesha baiskeli mkazi wa kijiji cha Kasharazi.
Watu waliofariki bado hawajatambuliwa na ndugu zao





No comments:
Post a Comment