ZAIDI YA WATU 700 WALIOOMBA KAZI KWENYE TAASISI MBALIMBALI WAMEITWA KWENYE INTERVIEW. MAJINA YAKO HAPA CLICK
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/I/122
09 MEI 2018
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Public Procurement Appeals Authority (PPAA), The National Institute for Medical Research (NIMR), National Institute of Transport (NIT), College of Business Education (CBE), The Mwalimu Nyerere Memorial Academy
(MNMA), Kibaha Education Centre (KEC), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa anapenda kuwataarifu waombaji kazi katika Taasisi zilizotajwa kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15-18 Mei, 2018 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Waombaji kazi wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili wa Mchujo unatarajiiwa kufanyika tarehe 15 - 18 Mei, 2018 kama ilivyoainishwa kwenye ratiba ya usaili kwenye tangazo hili.
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha uraia au hatibya kusafiria.
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na Vyeti Halisi vya kuanzia kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
v. Wasailiwa watakaokosa Vyeti halisi na badala yake kuwasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha IV na VI (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanya usaili.
viii. Kila Msailiwa afike na picha yake "passport size"
ix. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA)
x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.
RATIBA YA USAILI WA KUANDIKA (WRITTEN INTERVIEW), MAHOJIANO (ORAL INTERVIEW) NA ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA NA KADA ZAO ZIKO HAPA CLICK KUPAKUA PDF YENYE TAARIFA KAMILI.
No comments:
Post a Comment