Welcome to the word of the day, MARCH 27th, 2017. KWENU MABINTI
MABINTI..!
Upo tu kwenye uhusiano unataka hela ya Kusuka, hela ya kufanyia shopping, hela ya matumizi ya mwezi, kila shida ya Pesa uliyonayo unataka akutimizie.
Hivi upo kwenye Ndoa au upo kwenye uhusiano wa awali? Kama kwenye uhusiano tu unataka huduma zote hizo, ukiwa kwenye Ndoa itakuwaje?
Ni WAJIBU wa mwanaume kumtunza mkewe, kama anatimiza majukumu yake ya kukutunza kama mke wakati bado hampo kwenye Ndoa, Je na wewe upo TAYARI kumuhudumia kama Mume wa Ndoa?
Tamaa ya wanawake wengi ipo kwenye Pesa, na tamaa ya mwanaume ipo Katika kuifurahisha miili yao (kufanya ngono). Kama anakutimizia haja yako ya Pesa, Je upo tayar kumtimizia haja yake ya Mwili?
Unapenda kuchezea Pesa zake, Je upo tayar na yeye achezee Mwili wako?
Unapotaka KUPOKEA Ujue na KUTOA, Unapotaka KUVUNA basi ujue na KUPANDA, Ukiona VYAELEA Ujue VIMEUNDWA.
Acha Uvivu, Acha Kujiendekeza, Acha kutegemea vya kupewa, Acha kuwa Mzigo.
Jifunze KUJISIMAMIA, KUJITAFUTIA & KUJITEGEMEA, Jifunze KURIDHIKA
Mpenzi sio Baba yako wala mume wako..!
Kusaidiana kupo Lakini kuwe na KIASI.
MWANAMKE JITAMBUE.....!
Kwa taarifa zingine usikose kutembelea blog hii. Kisha share na wengine wapate tafadhali
1 comment:
Mabinti wengi huwa na tabia hizi lakini ni baadhi yao. Na kwa waliowapata nafikir wana raha sana. Vipi kwaki wewe?
Post a Comment