Beki wa FC BARCELONA arejea kikosini kuivaa Athletic Bilbao
Barcelona, Spain
Na Kalunde:Beki mahiri wa miamba wa Uhispania, FC Barcelona, Jordi Alba anatarajiwa kuingia kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa majeraha ya paja aliyoyapata kwenye mazoezi mapema mwezi huu.
Mhispania huyo akiwa anaugulia maumivu hayo, amekosa mechi tatu ambazo ni FC BARCELONA dhidi ya Olympiacos, Malaga na Murcia (ilikuwa mechi ya Copa Del Rey). Amerudi kwenye mazoezi Jumatano wiki hii na anatarajiwa kuivaa Athletic Bilbao hapo Jumamosi.
Kwa ujio wake Alba, Meneja wa timu hiyo Ernesto Valverde atakuwa na chaguzi sasa juu ya beki hawa. Lakini pia inasemekana Jordi Alba anafurahia sana kwenye uongozi wa kocha huyu mpya baada ya Luis Enrique.
Tembelea www.kalunde.co kwa habari mbalimbali pia
No comments:
Post a Comment