Huyu ndiye anashitakiwa kutaka kumpindua Rais Kagame, anasota lumande, anyimwa dhamana.
Rwanda
Mahakama nchini Rwanda imemnyima dhama mkosoaji mkuu wa Rais Paul Kagame na kuchelewesha kesi yake ya makosa ya kuchochea umma kuipindua serikali iliyoko madarakani. Jaji wa mahakama moja ya Kigali, amesema Diane Rwigara, mwanaharakati wa haki za wanawake, hawezi kupewa dhamana kwa sababu ya uzito wa makosa yanayomkabili. Adhabu ya makosa ya uchochezi hufikia hadi kifungo cha miaka 15 gerezani.
Mwezi Septemba, Anne, dada yake Diane pamoja na mama yao, Adeline walikamatwa pamoja na mkosoaji maarufu wa serikali na wote wanakabiliwa na makosa ya uhalifu. Jana Anne, anayeshutumiwa kwa kuiita Rwanda ''taifa la kimafia'' alipewa dhamana, huku mama yao naye akinyimwa dhamana. Rwigara ni mtoto wa Assinapol Rwigara, mfanyabiashara aliyekosana na Kagame kabla ya kifo chake kilichotokana na ajali ya gari mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment