#AJIRA: TANGAZO LA KUITWA KAZINI - MUHAS NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/J/68 13 Novemba, 2017
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) waliofanya usaili tarehe 3, 7 na 8 Novemba, 2017 kuwa matokeo ya usaili yamekwishaidhinishwa na waombaji kazi waliofaulu usaili huo na kupendekezwa kutumwa kwa Mwajiri ni kama yalivyoorodheshwa katika Tangazo hili.
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo Barabara ya Bibi Titi Mohamed, Jengo la Maktaba Kuu ya Taifa, ghorofa ya pili, Masjala ya wazi ndani ya siku 7 (kuanzia tarehe 15 Novemba, 2017), baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta. Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Original Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
No comments:
Post a Comment