Header Ads

##USAILI: KUITWA KWENYE USAILI KWENYE TAASISI MBALIMBALI; GPSA, PPRA, TBT, TAFIRI, ORCI, TEMESA, MNMA



JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.NaEA.7/96/01/J/66 13 Novemba, 2017
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mzinga Corporation , Government Procurement Services Agency (GPSA), Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), Tea Board of Tanzania (TBT), Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI), Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Tanzania Electrical, Mechanical and Services Agency (TEMESA), President’s Office, Ethics Secretariat na Mwalimu Nyerere Memorial Academy(MNMA) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili
unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 18-24 Novemba, 2017na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 18-23 Novemba,2017 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu usaili ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;

ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;

iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

v. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA); na

ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yaTangazo husika.

x. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

xi. Kwa waombaji kazi ambao watafanya usaili wa Mchujo tarehe 18 Novemba, 2017 katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere utaratibu wa vyumba vya kufanyia usaili kwa kila kada utatolewa kwenye tovuti (www.ajira.go.tz) kabla ya siku ya Usaili.
GUSA HAPA KUSOMA MAJINA, KADA YA TAREHE YA USAILI

No comments: