Header Ads

Kutoka Wizara ya Afya kuhusu ajira mwaka huu




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

TANGAZO LA KUITWA KAZINI.


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilipokea kibali cha kuajiri watumishi 3,152 wa kada mbalimbali za Afya nchini. Kibali hiki kilikuwa kwa ajili ya Wizara, Hospitali za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali. Maombi yalipokelewa kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi 31/08/2017.

Waombaji thelathini (30) wamechaguliwa na kupangiwa ajira Wizara ya Afya kama jedwali linavyoonesha kwenye Tovuti ya Wizara ya Afya, ili kuona majina ya waliochaguliwa ingia www.moh.go.tz

Waombaji 2,058 waliochaguliwa katika Hospitali za Mikoa na Halmashauri wametangazwa kwenye Tovuti ya OR TAMISEMI. Waombaji wote wanajulishwa kutembelea Tovuti hiyo www.tamisemi.go.tz. Aidha, Sekretarieti ya Ajira inaendelea kushughulikia ajira kwa Taasisi nyingine.

Waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa kuzingatia kwa ukamilifu maelekezo yafuatayo:-

Kuripoti Ofisi za Wizara ya Afya Dodoma katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ajira Serikalini. Ofisi za Wizara ya Afya zipo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii, Jengo namba 11.

Ambao hawataripoti ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa.

Wakati wa kuripoti kila aliyechaguliwa atapaswa kuwasilisha vyeti halisi (original Certificates) ambavyo nakala zake zilitumiwa wakati wa kuombea ajira zao. Hii ni pamoja na Vyeti halisi vya Elimu, vyeti vya Taaluma, Leseni kulingana na sifa za kada zao.

Awe na Cheti halisi cha Kuzaliwa (Original Birth Certificate) ambacho nakala yake aliambatisha kwenye maombi aliyowasilisha.

Mwombaji anatakiwa kuwa na picha mbili ndogo (passport size). Picha ziwe na muonekano kamili wa sura na ziwe zimepigwa si zaidi ya miezi mitatu.

Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
08/11/2017

No comments: