Header Ads

MKE ROBERT MUGABE, GRACE MUGABE AMEKIMBILIA NAMIBIA KUFUATIA MZOZO WA KISIASA NCHINI ZIMBABWE 🇿🇼





Mbunge kutoka chama cha upinzani nchini Zimbabwe, Eddie Cross amesema kuwa anaamini mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe, ametorokea Namibia baada ya kuwepo na hali ya wasiwasi. Mwanasiasa huyo wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema kuwa anafahamu kwamba, Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshila nchi hiyo. 

Ameongeza kuwa mke wa Rais Mugabe alikuwa hana sehemu nyingine ya kwenda kutafuta hifadhi baada ya kudaiwa kumdhalilisha mwanamitindo Afrika Kusini jambo ambalo lilimaanisha hatoweza kuomba hifadhi nchini humo kwani hatakuwa na usalama wa kutosha.

No comments: