Header Ads

MUGABE ASEMA YUKO TAYARI KUFA KWA KILICHO SAHIHI, APEWA MWISHO WA KUJIUZULU NI KESHO.

Amekataa kuachia ngazi


Rais Mugabe amepewa hadi kesho, Jumatatu mchana awe amekwisha andika barua ya kujiuzuru nafasi ya urais wakati Chama chake cha ZANU - PF pia kikiwa kimeshamuondoa katika nafasi ya kukiongoza na kumteua aliyekuwa makamu wake, Emmerson Mnangagwa.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, kupitia Dailymail, Rais Mugabe baada ya kupewa taarifa hiyo na kushuhudia maandamano ya jana, aliangua kilio na kumkumbuka mkewe marehemu Sally na mwanaye Michael Nhamodzenyika. 

Pia inadaiwa kuwa, Rais Mugabe tangu jana amegoma chakula, akisema " yuko tayari kufa kwa kile kilicho sahihi".

No comments: