Mwalimu Afariki baada ya Kupokea barua ya Uhamisho wa kwenda kufundisha shule ya msingi. Soma zaidi
Mwalimu Afariki baada ya Kupokea barua ya Uhamisho wa kwenda kufundisha shule ya msingi.
TANDAHIMBA, MTWARA: Mwalimu wa shule ya Sekondari Milongodi, anadaiwa kufariki dunia ghafla baada ya kupokea barua ya uhamisho wa kwenda kufundisha Shule ya Msingi
Inadaiwa alipata shinikizo la damu baada ya kupokea barua hiyo na kusababisha kupoteza maisha
Mnamo mwezi Mach 2017, Serikali ilisema itawahamisha walimu wa ziada katika masomo ya sanaa kwenye shule za sekondari wapatao 7,463 kwenda shule za msingi kupunguza upungufu na kuboresha elimu hiyo ya msingi
Aidha, Mwezi Januari 2018 Serikali kupitia kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda ilisema walimu wa sanaa watakaohamishwa kutoka shule za Sekondari kwenda kufundisha Shule za Msingi ni wale waliokuwa wanafundisha Shule za msingi awali kabla ya kujiendeleza
Chanzo: jamiiforums
No comments:
Post a Comment