Header Ads

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKAZI WA MAGU MWANZA AUAWA KIKATILI MKOANI IRINGA. TAARIFA YA POLISI IKO HAPA

Baadhi ya wanafunzi wakipatiwa msaada baada ya kuzimia na wengine kutojiweza kutokana na  kifo cha mpendwa wao

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA AUAWA:

Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato cha sita Sundi George mkazi wa wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza  aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari Mwembetogwa.

Mwanafunzi huyo alikutwa amefariki katika miti ya kugema pombe ya ulanzi huku mwili wake ukiwa na kamba shingoni.

Wanafunzi wakiwa katika hali ya majonzi makubwa sana kwa kuondokewa na mpendwa wao. 
Wanafunzi na wananchi wengine wakiuaga mwili wa Marehemu  

Akitoa taarifa za awali kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Juma Makanya amesema mnamo March 12 mwaka huu akiwa na sare za shule alitoka nyumbani kwao kuelekea shuleni lakini hakurudi hadi mwili wake ulipopatikana maeneo hayo.

Aidha kamanda bwire amesema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa kwa mtu yoyote wanayehi amehusika katika tukio hilo.
Chanzo: Azam 📺

No comments: