Miamba wa Uhispania, FC BARCELONA bado wanagugumia maumivu ya maajabu ya soka duniani,Barcelona ambao wametolewa katika michuano ya mabingwa wa Ulaya na klabu ya Roma kutoka Italia katika hatua ya robo fainali. Hatua ya kwanza ya mchezo huo Barcelona walishinda kwa 4 - 1 dhidi ya Roma na mchezo wa marudiano Barcelona wakishuhudia kichapo cha 3 - 0 kutoka kwa Roma na kuwa jumla ya magoli 4 - 4 lakini Roma walisonga mbele kwa faida ya goli moja la ugenini waliloifunga Barcelona.
Leo miamba hao walikuwa na mechi ya ligi kuu nchini Uhispania na wameshinda kwa 2 - 1 dhidi ya Valencia kiweka rekodi ya kucheza mechi 39 La Liga bila kupoteza.
Kwa matokeo hayo Barcelona wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo kama ifuatavyo. Soma taarifa hizi
No comments:
Post a Comment