Header Ads

#HABARI: WALIOFUTWA KAZI KWA SABABU YA KUWA NA ELIMU YA DARASA LA SABA KURUDISHWA KAZINI. CLICK HAPA


Serikali imetoa tamko Bungeni Kupitia Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. George H. Mkuchika la kuwarejesha kazini watumishi walioajiriwa wakiwa na elimu ya Darasa la saba walioachishwa kazi.

KAULI YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA BUNGENI LEO KUHUSU WATUMISHI WALIOONDOLEWA KWENYE MFUMO WA MALIPO YA MSHAHARA KWA KUKOSA SIFA YA CHETI CHA KUFAULU MTIHANI WA ELIMU YA KIDATO CHA NNE

Watumishi wote ambao na Ajira za Kudumu au Ajira za mikataba (Kwa Watendaji wa Vijiji na Mitaa) au ajira za muda (Employment on Temporary Terms) ambao walikuwa kazini kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ulipoanza kutumika Waraka wa utumishi( Establishment Circular) Na. 1 wa mwaka 2004, Warejeshwe kazini Mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria

Watumishi wa Umma Elfu Moja mia tatu sabini (1370) waliolegezewa masharti ya sifa za muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi yenye Kumb. Na. CCB.271/431/01/P/13 ya tarehe 30 Juni, 2011, warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria.

No comments: