TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO SHULE YA SEKONDARI MCHUNGAJI MWEMA (O'LEVEL & A'LEVEL). CLICK HAPA
| Baadhi ya wanafunzi katika mahafali ya kidato cha nne 2017 |
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO SHULE YA SEKONDARI MCHUNGAJI MWEMA (O'LEVEL NA A'LEVEL)
UTANGULIZI.
Shule ya Sekondari Mchungaji Mwema ni shule inayomilikiwa na Kanisa Anglikana Tanzania Dayosisi ya Kagera. Ni shule ya mchanganyiko (mseto) yaani wasichana na wavulana na wote ni Bweni (wanafunzi wa kulala tu).
Shule inawatangazia nafasi za kujiunga na masomo ya kidato cha TANO kwa mwaka wa masomo 208/2019 kwa tahasusi zifuatazo;
✍️ PCB (Physics, Chemistry, Biology)
✍️ CBG (Chemistry, Biology, Geography)
✍️ HGK (History, Geography, Kiswahili)
✍️HKL (History, Kiswahili, English Language).
✍️KLF (Kiswahili, English Language, French).
Masomo mengine yanayofundishwa kwa O'level ni: Civics, History, English Language, Kiswahili, French, Geography, Physics, Chemistry, Biology, Mathematics, na Bible Knowledge.
UFAFANUZI WA HUDUMA ZA KITAALUMA ZINAZOTOLEWA SHULENI KWA A'LEVEL
✍️Shule inatoa elimu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na masomo ya kidato cha tano kwa tahasusi za PCB, CBG, HGK, HKL na KLF 2018/2019.
✍️Shule inafundisha masomo ya ziada kwa watahiniwa wa kujitegemea kidato cha nne (PC) na wale wa Mtihani wa Maarifa (QT) kwa muda wa jioni, pia KITUO CHA WANAORUDIA MTIHANI KIPO.
✍️Kwa wanafunzi wanaotaka kusoma kidato cha TANO na hawana CREDIT, shule inawapa nafasi ya kuendelea na kidato cha TANO kwa tahasusi zao (combinations) huku wakijiandaa kurudia mitihani yao ya kidato cha nne ili kupata CREDIT.
SIFA ZA SHULE KWA UFUPI.
✍️Ada ya shule ni nafuu sana na unaweza kulipa ada hiyo kwa awamu kumaliza.
✍️Shule ina mandhari mazuri ya kuvutia, tulivu na rafiki kitaaluma.
✍️Shule ina maabara za masomo ya KEMIA, BIOLOJIA na FIZIKIA zinazomwezesha mwanafunzi kujifunza kwa vitendo.
![]() |
| Baadhi ya wanafunzi wakiwa maabara wakijifunza kwa vitendo. |
![]() |
| Baadhi ya wanafunzi wakiwa maabara wakijifunza kwa vitendo. |
✍️Shule ina umeme na maji muda wote.
✍️ Shule ina walimu wa kutosha wenye taaluma ya ualimu na uzoefu wa kumwezesha mwanafunzi afaulu masomo yake.
✍️ Shule ina mbinu bora na shirikishi zenye kumuwezesha mwanafunzi kuongea Kiingereza.
✍️ Shule inafanya vizuri kitaaluma katika mitihani ya kidato cha pili na Kidato cha nne kiwilaya, kimkoa na kitaifa.
✍️ Shule ya Sekondari Mchungaji Mwema inatoa malezi bora ya kiroho ikiwa ni malengo ya kumwandaa mwanafunzi kuwa na hofu ya Mungu, kuwajibika kwa vitendo, mbunifu, kujitegemea, kujiheshimu na kuheshimu wengine na mali na kuwa mtu muhimu katika jamii.
MALAZI YA SHULE
✍️Shule ina mabweni mapya na ya kisasa kabisa yenye huduma zote muhimu ndani (Self Contained). Kwa hiyo muda wa usiku hakuna haja ya mwanafunzi kutoka nje kupata huduma za choo na bafu, hii inamfanya mwanafunzi kuwa salama. Tazama picha za mabweni ya wanafunzi
| Mwonekano wa nje wa bweni la wavulana |
| Mwonekano wa bweni la wasichana kwa nje |
✍️Shule ya Sekondari Mchungaji Mwema inazingatia afya na lishe bora kwa mwanafunzi ili aweze kusoma vyema, ndio maana ikaamua kuanzisha bustani ya mbogamboga.
Tazama picha hapo chini.
MAHALI SHULE ILIPO.
Shule iko Mkoa wa Kagera Wilaya ya Ngara, kilometa 2 kutoka Makao Makuu ya Ngara barabara iendayo Bebaco - Mwanza, Kahama, Kigoma na Karagwe.
MAWASILIANO:
POSTA/BARUA.
Mkuu wa Shule,
Shule ya Sekondari Mchungaji Mwema,
S. L. P 08,
NGARA - KAGERA
SIMU:
0769 667 757
0714 155 626
0762 075 406
0682 038 468
E-MAIL:
![]() |
| Wageni kutoka nchi za nje waliotembelea Shule ya Sekondari Mchungaji Mwema na kupata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliokuwepo muda huo. |
| Wanafunzi kidato cha nne 2017 walipokuwa katika mahafali kwa furaha kabisa. |
| Muonekano wa shule kwa juu kutoka kwenye mlima. |






No comments:
Post a Comment