Header Ads

TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIOFANYA USAILI 19 - 20 MACHI, 2018. CLICK

Tangazo la kuitwa kazini


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/J/119 

10 Aprili, 2017
TANGAZO LA KUITWA KAZINI 


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu Waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 19 – 20 Machi, 2018 kuwa majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Data base) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo Barabara ya Bibi Titi Mohamed, Jengo la Maktaba Kuu ya Taifa, ghorofa ya pili, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka
tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazijachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.

Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

No comments: