ORODHA YA WAOMBAJI WALIODAHILIWA NA CHUO ZAIDI YA KIMOJA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/19. CLICK HERE
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia umma kuwa imekamilisha uhakiki wa sifa za waombaji waliodahiliwa na taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2018/19. Orodha za majina ya waombaji zilizowasilishwa Tume na vyuo kwa ajili ya uhakiki zimesharejeshwa vyuoni pamoja na matokeo ya uhakiki ili vyuo husika viweze kutangaza majina ya waliowadahili.
Hata hivyo, katika orodha hizo wako waombaji waliodahiliwa na vyuo zaidi ya kimoja. Orodha yao na vyuo walivyodahiliwa inapatikana kupitia tovuti ya Tume www.tcu.go.tz. Aidha, waombaji wa aina hii wamejulishwa kuhusu udahili wao kupitia ujumbe mfupi uliotumwa kwenye namba za simu za mikononi walizotumia wakati wa kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo husika.
Tume inapenda kuwatangazia wote waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja kuthibisha udahili katika chuo kimoja tu mwombaji anachopendelea kujiunga. Mwombaji anatakiwa kufuata utaratibu ufuatao:
1) Kunakili namba maalumu (special code) iliyotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi kwenye simu yake;
2) Kutumia nywila (password) kuingia katika profile yake iliyo katika
mfumo wa udahili wa chuo anachokipenda kati ya vile alivyodahiliwa;
3) Kuingiza namba hiyo maalumu katika mfumo wa udahili wa chuo ili kuthibitisha udahili wake katika chuo hicho; na
4) Kuthibitisha udahili wake katika chuo kimoja kabla ya terehe 5 Septemba 2018.
Tume inapenda kusisitiza kuwa, mwombaji atakayeshindwa kuthibitisha udahili wake katika muda uliopangwa, atapoteza nafasi yake na kulazimika kuomba upya katika awamu zitakazofuata.
Imetolewa na
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
01/09/2018
No comments:
Post a Comment