WALIOCHAGULIWA UDEREVA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA DAR ES SALAAM. ANGALIA JINA LAKO HAPA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
TANGAZO LA KUITWA KAZINI NAFASI YA UDEREVA
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi ya kazi ya Udereva kwa ajili ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali waliofanya usaili tarehe 03Oktoba, 2017 na kufaulu usaili huo kuwa wanatakiwa kufika bila kukosa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kilichopo jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi tarehe 9
Novemba, 2017 saa mbili kamili asubuhi.
Majina ya waliofaulu usaili huo yameainisha chini ya tangazo hili, kwa
wale watakaoona majina yao wafahamu kuwa wanatakiwa kwenda na Vyeti vyao halisi kuanzia cheti cha kidato cha nne, vyeti vya Udereva pamoja na nyaraka nyingine ikiwemo cheti cha kuzaliwa na kitambulisho.
Wakifika hapo (TPSC) watakuta barua zao za kupangiwa kituo cha kazi pamoja na maelekezo ya hatua zinazofuata kwa ajili ya kukamilisha taratibu zao za Ajira husika.
Aidha, kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Ifuatayo ni orodha ya majina ya Waombaji kazi waliofaulu usaili huo
wa nafasi za kazi ya Udereva 150 zilizokuwa zimetangazwa.
No comments:
Post a Comment