Kauli ya KMC FC kuelekea mechi yao dhidi ya Geita Gold FC
KMC FC KUWAKARIBISHA GEITA GOLD KESHO DIMBA LA CHAMANZI
Kikosi cha Timu ya KMC kesho kitashuka katika Dimba la chamanzi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold mchezo utakaopigwa saa 16:00 jioni.
Soma pia hapa wachezaji wa Simba waliobainika kuwa na COVID 19
Mchezo huo wa mzunguko wa nane utapigwa kesho huku KMC FC ikiwa mwenyeji na kwamba hadi sasa maandalizi yameshafanyika kwa asilimia kubwa na kikosi kiko tayari kwa mtanange huo.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu John Simkoko na wasaidizi wake Habibu Kondo pamoja na Hamad Ally imefanya maandalizi ya kutosha kabisa na kwamba malengo makubwa kwenye mchezo huo ni kuhakikisha kwamba kama Timu inapata ushindi.
Licha ya ushindani uliopo kwa Timu pinzani Geita Gold lakini bado kikosi kinamatumaini makubwa yakufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho na hivyo kuondoka na alama tatu muhimu ambazo kila mmoja anazihitaji.
"Kwa ujumla kikosi kipo vizuri, wachezaji wana Afya njema, wanamorali nzuri na kikubwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo tutakwenda kupabambania alama tatu.
"Maandalizi yetu kwa kiasi kikubwa yamefanyika vizuri, kwasababu tunajua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa sana, nasisi tunahitaji matokeo hivyo tutakwenda kupambana ukizingatia KMC ni Timu Bora nilazima tuendelee kuonyesha ubora wetu.
Unaweza pia kusoma >>Mkataba wa Morrison na Simba waelekea ukingoni.
Hadi Sasa KMC FC imecheza michezo Saba ambapo kati ya michezo hiyo imeshinda mmoja na kupoteza michezo mitatu huku ikitoka sare kwenye michezo mitatu na kujikusanyia jumla ya alama sita na magoli manne hadi sasa na kuwa kweye nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania.
Mwisho.
Imetolewa leo Disemba 4N
NaChristina Mwagala
Ofisa Habari na Mawasiliano KMC
No comments:
Post a Comment